TIRA (Tanzania Insurance Regularatory Authority) ni taasisi inayo husika na BIMA zote tanzania. Taasisi hii imeundwa mwaka 2009 kwa lengo la kusimamia mawakala wa bima kufanya kazi kwa viwango vinavyo takiwa.

Kwa upande wa magari kuna bima aina mbili ambazo ni third party na comprehensive.

Third party ni bima nafuu ambazo kawaida kwenye magari mengi huwaga haizidi 150000. Bima hii inakulinda wewe usipate madeni endapo utakua umegonga na kuaribu chombo cha mtu. Bima hii haitahusika na utengenezaji wa gari yako pindi umepata ajali

Comprehensive ni aina ya bima ya gharama kulinganisha na third party. Aina hii ya bima itaweza kukusaidia kutengeneza gari lako na la yule ambaye umemgonga. Makadirio ya gharama zake itategemeana na thamani ya gari lako au kiwango ambacho utataka ulipie kwa kuthaminisha gari lako.

Hali umeshaelewa hilo, basi unaweza tumia njia hii kujua gari hili kama bima yake inafanya kazi au laa. Vile vile utajua kiasi kilicho lipiwa na wakala alietumia kukata bima hio. Kwa taarifa hizo utajua kama ni comprehensive au third party ndio iliokatwa.

Bofya hapo chini kisha jaza taarifa za namba ya gari upate taarifa zake

https://tiramis.tira.go.tz/

Soma link hapo chini ujue kampuni 10 bora za bima zinazolipa haraka na pesa nzuri endapo utapata ajali

Bima ya Magari

https://www.dawazetu.co.tz/matokeo