Kitunguu saumu ni dawa na tiba ya magonjwa mengi sana. Kwa leo tutaongelea kitunguu saumu kutibu fangasi ukeni.
Mambo yanayotakiwa kufanya kutengeneza dawa ya kutibu fangasi ukeni ni yafuatayo;
Chukua kitunguu saumu chako kimoja tu, Kisha kimenye alafu chukua punje nane au kumi kwa uhakika zaidi. Zikatekate punje hizo kuwa vipande vidogo vidogo au visage kwenye brenda huku ukiwa umeweka maji kidogo.
Baada ya hapo kunywa maji hayo. Rudia Kitendo hichi kwa muda usio pungua wiki mbili. Endapo utaona mabadiliko makubwa ndani ya wiki moja na kuto ona fangasi tena, usiache tumia dozi hii. Endelea kutumia mpaka ifikapo wiki mbili.
Ukiacha kutumia dozi hii kabla ya muda wake, Utafanya fangasi hao wawe sugu na vigumu kutoka. Hivyo basi zingatia maelekezo vizuri uweze kupona.
Endapo utaona umetumia dozi hii kwa muda wa wiki tatu na hujapata mabadiliko au mafanikio yoyote, Kwa mazingira hayo itakulazimu uende hospitali mapema maana kitu hicho sio ishara nzuri.
You must Register or Login to post a comment