Habari wapendwa,
Je unatatizo la traffic barabarani na unahitaji kulipia deni la gari lako?
Au ulikua unataka kuhakikisha kama gari lako lina deni au laa?
Umepoteza karatasi ya kulipia fine ya gari lako kwaio unajiuliza utafanyaje uweze kulipia deni la gari lako?
Njia sahihi ni ku Bofya link ya hapo chini itakupeleka ukurasa wa kuweza kuandika namba ya gari lako na kuona kama linadaiwa au laa. Hii link itakuwezesha pia kupata control number kwa ajili ya kufanya malipo
Au Unaweza kujaza namba za Gari lako hapo kwenye Jedwali kisha bonyeza Search utapata matokeo ya chombo chako
Jinsi ya kulipia deni la gari kwa njia ya Simu
Endapo utakua umekagua namba ya gari lako na kukutana na fine ambayo inatakiwa kulipwa, Unaweza tumia njia ya rahisi ya simu kufanya malipo na kuondoa deni lako
- Fungua menu ya malipo kama ni Airtel Money, M-pesa, tigo pesa au halo pesa
- Chagua namba inayo husiana na kulipia bili
- Mitandao mingine itakupa menu ya kuweza kuweka namba ya kampuni ambapo ukichagua utajaza 001001 baada ya hapo utajaza kumbukumbu namba ambayo ipo kwenye receipt ya faini au TMS uliopata online [ https://tms.tpf.go.tz/]
- Mitandao mingine itakupa option ya kujaza kumbukumbu namba mwishoni kujaza namba ya kampuni. Kwenye kumbukumbu namba jaza namba ya receipt ya TMS kwenye namba ya kampuni jaza 001001
- Baada ya hapo jaza kiasi cha malipo
- Mwisho kabisa weka namba ya siri. Deni lako litakuwa limefutika
Kwa maelezo zaidi piga simu namba 0677038217
Richard
6:54 am at 6:54 am
Hii blog ni nzuri imenisaidia kwa namna flani. Ile risiti nilipoteza kupitia nyie nimepata ile namba ya kumbu kumbu. Asanteni sana
David
6:56 am at 6:56 am
Mmefanya vzuri maelezo yenu naona yanajitosheleza kabisa. Natumia mtandao wa tigo nimeweza kulipia deni bila wasiwasi.
Rashidi
7:11 am at 7:11 am
Mimi natumia mtandao wa Airtel mbona nikishachagua lipa bili af nikienda chagua kampuni sioni sehem ya traffic au kujaza namba yao ya kumbukumbu namba. Napata makampuni mengine tu. Nimekwama apo. Inatakiwa kufanyaje
admin
7:19 am at 7:19 am
Mr. Rashidi kama unatumia mtandao wa Airtel kufanya malipo, ukishafungua lipa bili chagua malipo ya serikali baada ya hapo chagua kumbukumbu namba kisha jaza ile control number ambayo umepata kwenye TMS au risiti yako. Endelea mbele kujaza kiasi unacholipia baada ya hapo utaona maelekezo ya kwamba unalipia kwenye namba ya kampuni 001001. utakua umeshafanikiwa ukifatisha vizuri step zinazofata
James
7:23 am at 7:23 am
Aisee shukrani sana mm natumia mtandao wa tigo hizo step mlizo weka hapo zipo sahihi kabisa. Nimejaribu kuangalia tena baada ya kufanya malipo naona deni limeondoka kabisa. Halipo tena. Shukrani sana
Joseph
7:25 am at 7:25 am
Mitandao ina rahisisha sana mambo sikuizi. Mtu unaweza ukawa umekaa unawaza kitu flani utakifanyaje ukiuliza hata jirani yako hajui namna ya kukusaidia ila nimeona kwa kupitia mitandao sikuizi mambo yamekua rahisi mno. Shukran watu wa luisguide. Nimeweza kulipia deni la gari langu
ABDULKALIM JIMMY
10:23 am at 10:23 am
Mm nataka nipate APP ya kuangalia hayo maden na fine nazodaiwa
admin
7:28 am at 7:28 am
Haina haja ya kuwa na app. Ukisoma kwenye hayo maelekezo ukibonyeza hio link ya TMS unakua unaweza kujaza namba ya gari na kuona kila kitu.